Rekodi mbaya ya Liverpool dakika za Jioni EPL
Sisti Herman
March 4, 2026
Share :

Msimu wa Liverpool katika Ligi Kuu ya Uingereza umegubikwa na jinamizi linalojirudia katika dakika za lala salama za michezo yao.
Msimu huu pekee, "Majogoo" hao wamepata vipigo mara tano katika ligi kutokana na kuruhusu mabao katika dakika ya 90 au zaidi.
Tabia hii ya kupoteza umakini wakati filimbi ya mwisho ikikaribia imekuwa na gharama kubwa, ikiwapotezea pointi muhimu na kuibua maswali mazito kuhusu umakini wa safu yao ya ulinzi na namna wanavyoweza kudhibiti mchezo wakiwa chini ya shinikizo.





