Rekodi saba alizofikia na kuzivunja Messi baada ya kukipiga na Algeria.
Joyce Shedrack
June 17, 2026
Share :
Lionel Messi ameweka historia nyingine kubwa baada ya kuiongoza Argentina kushinda 3-0 dhidi ya Algeria katika mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Dunia la FIFA 2026. Katika mechi hiyo, Messi alifunga mabao yote matatu (hat-trick) na kuvunja au kufikia rekodi saba muhimu.

Rekodi Alizovunja au Kufikia Lionel Messi
1:Mabao Mengi Zaidi ya Kombe la Dunia: Amemfikia Miroslav Klose kwa kufunga jumla ya mabao 16 kwenye historia ya mashindano haya.
- 2;Kushiriki Kombe la Dunia Mara Sita: Amekuwa mchezaji wa kwanza wa kiume kucheza katika mashindano 6 tofauti ya Kombe la Dunia (2006–2026).
- 3;Mchezaji Mkongwe Zaidi Kufunga Hat-Trick: Ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kufunga mabao matatu kwenye mechi moja ya Kombe la Dunia akiwa na umri wa miaka 38.
- 4;Mchango Mkubwa Zaidi wa Mabao: Amefikisha jumla ya mabao na pasi za mabao (assists) 24, akivunja rekodi ya awali ya Pelé (21).
- 5;Kufunga Mechi Tano Mfululizo: Amekuwa Mwargentina wa kwanza kufunga katika mechi 5 mfululizo za Kombe la Dunia.
- 6;Mabao Mengi Kutokea Nje ya Sura ya Penati: Amemfikia Rivellino wa Brazil kwa kufunga jumla ya mabao 5 kutokea nje ya kisanduku cha hatari tangu mwaka 1966.
- 7;Mechi 200 za Kimataifa: Amefikisha jumla ya mechi 200 akiichezea timu yake ya taifa ya Argentina.





