Rekodi zazidi kumfuata Mainoo alikua Liver
Sisti Herman
April 7, 2024
Share :
Akiwa na miaka 18 tu, kinda wa Manchester United Kobbie Mainoo rekodi zimezidi kumfuata msimu huu mara baada ya leo kufunga goli lake la kwanza kwenye dimba la Old Trafford akiwa na uzi wa timu kubwa ya United kwenye dabi ya kihistoria ya ligi kuu Uingereza dhidi ya Liverpool wakitoa sare ya 2-2.
Huu umekuwa mwaka wa mafanikio kwa Kobbie mara baada ya kupandishwa timu kubwa akitokea timu ya vijana ambapo mpaka sasa amecheza mechi 17 za ligi na kufunga mabao mabao mawili, huku pia akiitwa timu ya Taifa ya Uingereza na Kucheza michezo miwili ya kirafiki.
Mabao mengine ya Mchezo huo yakifungwa na Bruno Fernandes (Utd) huku kwa upande wa Liverpool yakifungwa na Mohamed Salah na Luis Diaz.