pmbet

Rhulani Mokwena awaonya mashabiki wa Wydad,

Joyce Shedrack

June 22, 2024
Share :

Kocha Mkuu wa Mamelodi Sundowns Rhulani Mokwena amewataka mashabiki wa Wydad Casablanca kuacha kumtupia lawama kiungo fundi na nahodha wa timu hiyo Yahya Jabrane huku akimmwagia sifa kiungo huyo kuwa ni kiungo bora Afrika.

 

Mokwena amefunguka hayo katika kipindi maalumu alichofanya asubuhi ya leo kwenye moja ya chombo cha habari huko Afrika Kusini na  kusema Yahya Jabrane anapaswa kupewa heshima ni mchezaji mzuri.

“Yahya Jabrane ni mchezaji ninayempenda zaidi Wydad kwa sababu ni mchezaji bora, kwenye kiungo, na ni miongoni mwa wachezaji bora zaidi barani Afrika,

Mashabiki hawapaswi kulalamika sana juu ya mchezaji mzuri kama huyo. Ni klabu nzima inayoteseka na Jabrane hapaswi kuwa pekee na kutengwa. Mashabiki wasisahau alichotoa kwa klabu hii nzuri.”Amesema Mokwena

 

Ikumbukwe  Klabu ya Wydad imekuwa na msimu mbaya zaidi msimu huu kwenye Ligi Kuu ya Morocco na mashindano mengine ukitajwa kuwa msimu mbovu zaidi kwa miaka ya hivi karibuni kutokana na kuishia hatua ya makundi kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika na kumaliza nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi kuu Morocco huku mashabiki wakimtafuta wa kumtupia lawama.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet