Rick Ross atoa formula ya kuendelea kubaki tajiri
Eric Buyanza
December 11, 2023
Share :
MwanaHiphop kutoka nchini Marekani Rick Ross anasema ili uweze kubaki na utajiri wako ni vyema ukawawezesha watu wanaokuzunguka, akimaanisha familia.
“Watu wa familia yangu hawajaniomba chochote kwa miaka mingi. Mama yangu ni milionea. Dada yangu pia ni milionea. Niliwawezesha na wanajiweza. Kuwezesha wanaokuzunguka,kuwezesha familia yako ndio ufunguo bora wa kukufanya uendelee kubaki tajiri. Ikiwa wewe ni tajiri na kila mtu aliye karibu yako ni maskini, haitakuchukua muda wewe kurudi tena kwenye umaskini"