Rick Ross azawadiwa bunduki akisherekea siku yake ya kuzaliwa.
Joyce Shedrack
January 30, 2025
Share :
Rapa na mwanamuziki maarufu wa Marekani Rick Ross amezawadiwa bunduki aina ya "1911 vault" siku ya jana na rafiki yake akiwa anasherekea siku yake ya kuzaliwa.

Msanii huyo ambaye ametimiza miaka 49 alifanya sherehe ndogo iliyohudhuriwa na baadhi ya watu ndipo rafiki yake anayeitwa Freddy akamkabidhi zawadi ya Silaha hiyo.
Rick Ross amechapisha video kwenye ukurasa wake wa Instagram akimshukuru rafiki yake huku akisema ni zawadi nzuri kwa ajili ya kujitengenezea amani.