Rick Ross kununua hakimiliki ya nyimbo za 50 Cent!
Eric Buyanza
December 12, 2023
Share :
Rapa wa Marekani, Rick Ross "Rozay" ametoa ofa ya Dola Milioni 1.5 (zaidi ya Tsh Bilioni 3.7/=) kwa 50 Cent ili kununua hakimiliki za nyimbo za wasanii wake wa G-Unit ambao ni Young Buck, Llyoyd Banks pamoja na Tony Yayo.
Lakini pia amesema ataongeza Dola laki 5 (zaidi ya Tsh Bilioni 1.1/=) kwa 50 Cent ili aweze kuinunua album ya G-Unit iitwayo "Beg For Mercy"