Rihanna afunika tumbo kwa flana ya 'Nimestaafu', anatarajia mtoto wa 3
Eric Buyanza
June 8, 2024
Share :
Nyota wa muziki wa RnB, Rihanna, amenaswa na kamera za wanahabari katika jiji la New York wiki hii akiwa amevalia tisheti iliyoandikwa 'I'm Retired' (Nimestaafu) huku akificha tumbo lake nyuma ya mkoba, wengi wakisema anaficha ujauzito...kwani kuna uwezekano mkubwa staa huyo akawa anatarajia mtoto wake wa tatu.
Kitendo cha kuvaa tisheti ya kustaafu na huku kukiwa na uwezekano mkubwa wa yeye kuwa mjamzito, sauti za mashabiki wake zimesikika kila kona ya dunia wakiwa wamekata tamaa ya kupokea albam mpya kutoka kwa msanii huyo kwa siku za karibuni.
Mashabiki wa Rihanna wamekuwa wakisubiri kwa hamu kazi mpya za msanii huyo kwa muda mrefu sasa, ikumbukwe albamu yake ya mwisho (Anti) ilitoka January 28 mwaka 2016.