pmbet

Rio Ferdinand alipigwa sindano ili aweze kucheze Man U.

Joyce Shedrack

February 10, 2026
Share :

Rio Ferdinand, beki wa zamani wa Manchester United, anaendelea kukumbwa na matatizo ya kiafya kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye kazi yake ya soka.
Man Utd return could hold appeal to ex-captain Rio Ferdinand: 'It all  depends on the shape of the job' | London Evening Standard | The Standard

Mkongwe huyo kwa sasa ana umri wa miaka 47 lakini bado anapata matibabu ya mara kwa mara kutokana na maumivu ya mgongo na majeraha mengine.

 

Ferdinand alisema kwenye mahojiano na Men’s Health UK kuwa amekuwa akipata matibabu kwa muda mrefu, ikiwa ni pamoja na matumizi ya dawa za kutuliza maumivu na sindano kwa miaka sita mfululizo ili aweze kucheza mechi.

 

“Nilikuwa na maumivu makubwa, lakini nililazimika kuendelea kucheza. Sasa, ninapata matibabu ya mara kwa mara ili kupunguza maumivu,” alisema Ferdinand.

 

Ferdinand alikuwa mmoja wa mabeki bora wa wakati wake, akicheza mechi 504 kwa Manchester United na kushinda mataji mengi, ikiwa ni pamoja na mataji sita ya Ligi Kuu ya Uingereza na moja la Ligi ya Mabingwa ya UEFA.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet