RIPOTI YA UN: TTP ni kundi kubwa zaidi la kigaidi
Eric Buyanza
July 13, 2024
Share :
Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inasema Tehrik-i-Taliban Pakistan (TTP), muungano wa makundi yenye itikadi kali, ni kundi kubwa zaidi la kigaidi Afghanistan na linaungwa mkono zaidi na watawala wa Taliban kufanya mashambulizi ya kuvuka mpaka wa Pakistan.
VOA inaripoti kuwa timu ya waangalizi wa vikwazo ya Umoja wa Mataifa ilitoa tathmini hiyo wiki hii wakati kukiwa na ongezeko kubwa la mashambulizi ya kigaidi yanayoongozwa na TTP dhidi ya vikosi vya usalama vya Pakistani na raia, na kuua mamia yao katika wiki za hivi karibuni.
Ilibainisha kuwa kundi lililotangazwa kimataifa kuwa la kigaidi na kujulikana pia kama Taliban wa Pakistani, linaendesha shughuli zake nchini Afghanistan likiwa na wastani wa wapiganaji kati ya 6,000 na 6,500.