Robinho kutumikia miaka 9 jela kwa kosa la ubakaji
Eric Buyanza
March 22, 2024
Share :
Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Brazil Robinho amekamatwa ili kutumikia kifungo cha miaka tisa jela kwa kosa la ubakaji alioufanya mwaka 2013 huko Milan nchini Italia dhidi ya mwanamke wa Kialbania katika klabu ya usiku.
Robinho, mwenye umri wa miaka 40, alikamatwa akiwa nyumbani kwake katika jiji la Santos.
Hatua hiyo imesifiwa na wabrazil wengi ambao walihofia kwamba Robinho angekwepa adhabu kutokana na utajiri wake na umaarufu alionao.