Rodri apania ubingwa wa UEFA akiwa na uzi wa Barcelona.
Joyce Shedrack
August 17, 2026
Share :
Kiungo wa Hispania Rodri ameonyesha kiu kubwa ya mafanikio baada ya kuwasili Nchini Hispania kujiunga na Barcelona akisema yuko tayari kutoa kila kitu katika harakati za kuwania mataji yote msimu huu.

“Nina furaha sana kuwa hapa. Ninasubiri kwa hamu kufanya kazi na wachezaji wenzangu na kutoa uwezo wangu wote. Kwa sasa ninaishi ndoto yangu.”
Kiungo huyo ameweka wazi kuwa lengo lao si taji moja pekee, bali wanataka kupigania kila kitu, akilitaja pia taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kama moja ya malengo makubwa.
“Tutaenda kuipigania Ligi ya Mabingwa tutaenda kupigania kila kitu.” Amesema Rodri.





