Rodri aumiza kichwa cha Guardiola
Eric Buyanza
December 8, 2023
Share :
Takwimu za ligi kuu Uingereza zinaonyesha kuwa baada ya michezo 15 hadi sasa tayari Manchester City wamepoteza michezo minne, huu ni mwanzo mbaya wa msimu tangu kufika kwa kocha Pep Guardiola kwenye klabu hiyo.
Moja kati ya sababu kubwa kwa kuanza msimu vibaya kwa City ni kuwakosa baadhi nyota wao muhimu kama Kelvin De Bruyne huku athari kubwa ikiwa mechi kumkosa kiungo wa mzuiaji Rodri ambaye mpaka sasa amekosa michezo minne na ndiyo hiyohiyo City waliyopoteza.
Guardiola ameonekana kuwajaribu viungo na mabeki wakati tofauti kwenye nafasi ya Rodri bila mafanikio.