Rodriguez kama kazaliwa upya Copa-America
Sisti Herman
June 25, 2024
Share :
Kama ulidhani James Rodriguez ameisha basi jitahidi uamke alfajiri uone makeke yake,ndiyo kiungo huo mshambualiaji wa zamani wa Real Madrid na Bayern Munich alfajiri ya leo alipika mabao mawili makali yaliyoipa ushindi timu yake ya Taifa ya Colombia dhidi ya Paraguay kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya kombe la mataifa ya America (Copa America), Colombia wakishinda 2-1.
Rodriguez mwenye umri wa miaka 32 alipika mabao kwa beki wa kulia Daniel Munoz kwa krosi kali dakika ya 32 na dakika 10 baadae akapika lingine kwa faulo aliyopiga iliyomaliziwa na Kiungo wa kati Jefferson Lerma dakika ya 42 kukamilisha ushindi huo huku bapo la pekee la kufutia machozi la Paraguay likifungwa na Julio Enciso dakika ya 69.
Colombia wanaongoza msimamo wa kundi B wakiwa na alama 3 wakifuatiwa na Brazil na Costa-rica walitoa sare ya 0-0, huku Paraguay wakiburuza mkia wa kundi.