Roma hakuja Bongo wala Chidi hakuenda U.S.A, ni utndu wangu tu
Sisti Herman
January 14, 2024
Share :
Muongozaji wa video ya wimbo wa Roma Mkatoliki aliomshirikisha Chidi Benz inayokwenda kwa jina la “Nasikia harufu”, Director Black X amefichua kuwa kwenye video hiyo hakua Roma aliyekuja Tanzania wala Chidi Benz kwenda Marekani bali walifanya utundu kuweza kufanya mastaa hao wa Hip Hop waonekane kwenye video moja.
“Pale ni ufundi tu wa kuhariri video, Chidi Benz hakusafiri kwenda U.S.A wala Roma hakuja Tanzania” alisema Black X
Video hiyo ambayo ina siku 10 ipo namba 1 kwenye video zinazo trend kwenye mtandao wa Youtube kwa siku ya 8 mfululizo.