pmbet

Ronaldo aandika rekodi mpya ua ufungaji wa mabao Saudia

Sisti Herman

May 28, 2024
Share :

Nahodha na mshambuliaji kinara wa klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia Cristiano Ronaldo ameendeleza ubabe katika ligi kuu nchini humo baada ya kuweka rekodi mpya ya kufunga mabao mengi katika msimu mmoja baada ya kufunga mabao mawili kwenye mechi dhidi ya Al Ittihad.

Kupitia mechi hiyo Ronaldo aliweka rekodi ya kufikisha mabao 35 ndani ya msimu 2023/24 na kuipiku rekodi ya awali ya mabao 34 iliyowahi kuwekwa na Abderrazak Hamdallah msimu wa 2018/19.

Mafanikio haya yameendelea kumeweka pazuri Ronaldo katika maisha yake ya ‘soka’ licha ya kukaribia kufikia miaka 40 huku baadhi ya wanasoka wakidaiwa kuiga jitihada za nyota huyo ili kufikia ‘levo’ yake.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet