pmbet

Ronaldo aendelea kutesa duniani, amzidi Messi mapato mara mbili

Eric Buyanza

October 21, 2026
Share :

Ushindani wa miaka mingi kati ya magwiji wa soka duniani, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, umechukua sura mpya, safari hii si uwanjani bali kwenye akaunti zao za benki. Ripoti mpya ya kifedha kutoka jarida maarufu la Forbes imethibitisha kuwa makadirio ya mapato ya Ronaldo sasa yanazidi mara mbili ya yale ya nahodha wa Inter Miami, Lionel Messi.
 

Kulingana na mchanganuo wa Forbes kuhusu wachezaji soka wanaolipwa fedha nyingi zaidi duniani kwa mwaka huu, Ronaldo, anayekipiga katika klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia, anaongoza orodha hiyo kwa kuingiza jumla ya dola milioni 300 (takriban shilingi bilioni 830 za Kitanzania).

Kwa upande mwingine, mpinzani wake wa karibu, Lionel Messi, anashika nafasi ya pili akiwa na jumla ya mapato ya dola milioni 145 (takriban shilingi bilioni 400 za Kitanzania), kiwango ambacho ni chini ya nusu ya anachoingiza Ronaldo.
 

Licha ya wachezaji wote wawili kuelekea ukingoni mwa taaluma zao za soka wakicheza nje ya Ulaya, uwezo wao wa kutengeneza fedha unaendelea kuvunja rekodi na kuwaacha mbali wachezaji wa kizazi kipya.


HII HAPA LISTI YA WACHEZAJI SOKA 10 WANAOLIPWA ZAIDI DUNIANI KWA MWAKA 2026;
 

๐Ÿญ.๐Ÿ‡ต๐Ÿ‡น Cristiano Ronaldo โ€” ๐—จ๐—ฆ๐—— $๐Ÿฏ๐Ÿฌ๐Ÿฌ๐— 
๐Ÿฎ. ๐Ÿ‡ฆ๐Ÿ‡ท Lionel Messi โ€” ๐—จ๐—ฆ๐—— $๐Ÿญ๐Ÿฐ๐Ÿฑ๐— 
๐Ÿฏ. ๐Ÿ‡ซ๐Ÿ‡ท Kylian Mbappรฉ โ€” ๐—จ๐—ฆ๐—— $๐Ÿญ๐Ÿฌ๐Ÿฌ๐— 
๐Ÿฐ. ๐Ÿ‡ณ๐Ÿ‡ด Erling Haaland โ€” ๐—จ๐—ฆ๐—— $๐Ÿด๐Ÿฑ๐— 
๐Ÿฑ. ๐Ÿ‡ง๐Ÿ‡ท Vinรญcius Jรบnior โ€” ๐—จ๐—ฆ๐—— $๐Ÿณ๐Ÿฒ๐— 
๐Ÿฒ. ๐Ÿ‡ช๐Ÿ‡ธ Lamine Yamal โ€” ๐—จ๐—ฆ๐—— $๐Ÿฑ๐Ÿฑ๐— 
๐Ÿณ. ๐Ÿ‡ธ๐Ÿ‡ณ Sadio Manรฉ โ€” ๐—จ๐—ฆ๐—— $๐Ÿฑ๐Ÿฐ๐— 
๐Ÿด. ๐Ÿด๓ ง๓ ข๓ ฅ๓ ฎ๓ ง๓ ฟ Jude Bellingham โ€” ๐—จ๐—ฆ๐—— $๐Ÿฐ๐Ÿฑ๐— 
๐Ÿต. ๐Ÿด๓ ง๓ ข๓ ฅ๓ ฎ๓ ง๓ ฟ Harry Kane โ€” ๐—จ๐—ฆ๐—— $๐Ÿฐ๐Ÿฎ๐— 
๐Ÿญ๐Ÿฌ. ๐Ÿ‡ช๐Ÿ‡ฌ Mohamed Salah โ€” ๐—จ๐—ฆ๐—— $๐Ÿฐ๐Ÿฌ๐— 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet