Ronaldo afikisha goli 50 ndani ya mwaka mmoja
Eric Buyanza
December 12, 2023
Share :
Mshambuliaji wa Al Nassr na timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amefanikiwa kufikisha mabao 50 ndani ya kalenda ya mwaka 2023 huku akiwa hajamaliza mwaka.
Kupitia mitandao yake ya kijamii, Ronaldo alishapisha nukuu inayosema "nikiwa na umri wa miaka 15 nilimwambia mmoja kati ya wachezaji wenzangu kwenye mazoezi ya timu za vijana kuwa nitakuja kuwa mchezaji bora siku moja" akamaliza kwa kuandika "mfungaji bora wa muda wote kwenye historia ya mpira wa miguu, Asanteni"
Hii ni mara ya 8 Ronaldo kufikisha idadi hiyo ya mabao ndani ya kalenda ya mwaka mmoja.