Ronaldo ahofiwa kuchanika nyama za paja
Sisti Herman
March 1, 2026
Share :

Katika hali inayotia wasiwasi kwa wapenzi wa soka, inaripotiwa kuwa Cristiano Ronaldo amelazimika kuondoka uwanjani mapema kwenye mchezo wa leo dhidi ya Al Fayha.
Nyota huyo wa Kireno alionekana kupata jeraha la misuli ya paja (hamstring) wakati mchezo ukiendelea, jambo lililomfanya ashindwe kuendelea.
Madaktari walionekana wakimpatia huduma ya kwanza uwanjani kabla ya kufanyiwa mabadiliko, hali inayozua hofu juu ya ushiriki wake katika mechi zijazo huku klabu ikisubiri vipimo zaidi ili kubaini ukubwa wa tatizo hilo.
Kwenye mchezo huo timu yake imeshinda 3-1, huku yeye akikosa mkwaju wa penalti mapema.





