Ronaldo aitwa Timu ya Taifa akiwa na miaka 41.
Joyce Shedrack
September 18, 2026
Share :
Nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo, ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa na kocha Jorge Jesus kwa ajili ya michezo ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya kwa ajili ya michezo dhidi ya Wales, Norway na Denmark, huku akiwa tayari amefikisha umri wa miaka 41.
Ronaldo alianza kuitumikia timu ya taifa ya Ureno akiwa na umri wa miaka 18, akicheza mechi yake ya kwanza tarehe 20 Agosti 2003 dhidi ya Kazakhstan.
Zaidi ya miongo miwili baadaye, Ronaldo bado anaendelea kuwa sehemu muhimu ya timu hiyo akiwa amecheza jumla ya mechi 233 kwa Ureno na kufunga mabao 146 rekodi inayomfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wenye historia kubwa zaidi katika soka la kimataifa.





