pmbet

Ronaldo ampongeza Clara kutwaa ubingwa na kuongoza ufungaji

Sisti Herman

March 16, 2024
Share :

Klabu ya Al Nassr ya wanawake anayocheza nyota wa Tanzania Clara Luvanga imetwaa ubingwa wa ligi kuu wanawake nchini Saudi Arabia mara baada kushinda mchezo wao dhidi ya Al Hilal kwa goli 4-2 huku Clara akitupia moja nyavuni.

Hadi sasa Al Nassr wamecheza michezo 11 na kufikisha alama 31 huku wakibakiza michezo mitatu tu kukamilisha ratiba ya ligi kwani katika michezo hiyo Al Nassr wamezoa alama 31 huku timu inayowafuatia ikiwa na alama 18 na kushindwa kuwafikia kwa idadi ya michezo iliyobaki.

Clara Luvanga anaongoza mbio za ufungaji bora akilingana mabao na mshambuliaji Ibtissam wote wakiwa na magoli 10 huku Clara akimzidi mshindani wake kwa usaidizi wa mabao akiwa na asisti 3 hadi sasa Ibtissam hana asisti hata moja.

Kupitia mtandao wa instagram wa nyota wa Al Nassr Cristiano Ronaldo amewapongeza timu hiyo ya wanawake kupitia insta story yake.

Hilo linakuwa taji la kwanza kwa Clara Luvanga kwenye ligi alizowahi kucheza kwenye maisha yake ya soka, Kwa msaada wa ukurasa wa kuifadhi takwimu na rekodi mbalimbali za soka la wanawake Tanzania uitwao Matukio Muhimu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet