Ronaldo amponza Kigogo wa Serikali
Eric Buyanza
December 9, 2023
Share :
Gavana Nagasaki nchini wa Japan, aitwaye Kengo Oishi ambaye alienda kumuona Cristiano Ronaldo akicheza katika mechi kati ya Al Nassr FC na PSG Julai 25, huku akiacha kuhudhuria mkutano wa magavana aliopaswa kuhudhuria ametakiwa kujiuzulu.
Gavana huyo Julai 25, aliacha mkutano wa magavana na kwenda kutazama mchezo huo na baadaye akashiriki katika hafla baada ya mchezo na nyota huyo wa Ureno jambo ambalo baadhi ya watu wamelitafsiri kama matumizi mabaya ya madaraka.
Kutokana na kutakiwa kujiuzulu Gavana huyo amejitetea kwa kudai kuwa alitumia pesa zake mwenyewe kununua 'tiketi' ya mechi hiyo, ingawa gharama za usafiri na malazi ziligharamiwa na serikali ya Mkoa.
Pia amejitetea kuwa alitumia mkutano huo kumuomba Ronaldo kusaidia kulitangaza Jimbo lake la Nagasaki.