pmbet

Ronaldo 'amshtukiza' mama yake kwa zawadi ya gari aina ya Porsche

Eric Buyanza

January 2, 2024
Share :

Cristiano Ronaldo alihakikisha mama yake anaumaliza mwaka 2023 kwa style ya kipekee baada ya kuamua kumzawadia gari mpya aina ya Porsche kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa kwenye Mkesha wa Mwaka Mpya.
 

Dolores Aveiro, alikuwa anafikisha umri wa miaka 69 na staa huyo wa Ureno akarudi katika mji aliozaliwa wa Madeira kusherehekea pamoja naye.
 

Gari lilikuwa limefungwa kwa utepe mkubwa mwekundu, Aveiro alionekano akiwa na furaha zenye hisia kali huku akiwa amemkumbatia mjukuu wake kabla ya kuingia kwenye gari kwa mara ya kwanza.
 

Kisha alionyeshwa kwa ufupi jinsi gari hilo linavyofanya kazi, huku familia yake, akiwemo Ronaldo mwenyewe, wakitazama.
 

Dada yake Ronaldo aitwae Katia, alimsifu kaka yake kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa zawadi aliyompa  mama yao kwa kuandika........."Ikiwa ana furaha, ni kwa sababu mtoto wake anamkumbuka na si kwa sababu ya thamani ya zawadi......Waheshimu baba na mama yako upate siku nyingi za kuishi duniani"
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet