Ronaldo amvuta Casemiro Suadia
Sisti Herman
January 24, 2024
Share :
Klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia imetuma ofa ya kumsajili kiungo mkabaji wa Manchester United na timu ya taifa Brazil, Casemiro usajili ambao inasemekana unashinikizwa sana na mshambuliaji wa timu hiyo Cristiano Ronaldo.
Mbali na Casemiro pia Al Nassr inahitaji huduma ya rafiki mwingine wa Ronaldo kutoka United, beki Mfaransa Raphael Varane.