Ronaldo apigwa "chini" safari ya Uzbekistan
Eric Buyanza
November 2, 2026
Share :

Kocha mkuu wa Al-Nassr, Ange Postecoglou, amethibitisha kuwa amemwacha nahodha na mshambuliaji nyota wa timu hiyo, Cristiano Ronaldo, katika safari ya kuelekea Tashkent nchini Uzbekistan kukabiliana na Pakhtakor FC.
Postecoglou ameeleza kuwa uamuzi huo umetokana na mkakati wa kupunguza uchovu na kulinda usalama wa wachezaji kutokana na mlundikano mkubwa wa ratiba ya mechi na safari za mara kwa mara. Kando na Ronaldo, wachezaji wengine nyota kama Kingsley Coman na Mohamed Simakan nao wamepumzishwa na hawakusafiri na timu.
Kocha Postecoglou alisisitiza kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa uamuzi huo ni wa kupokezana vijiti ili kuwakinga wachezaji na uchovu mkubwa wa safari.
Ronaldo anaacha pengo kubwa kwenye kikosi hicho cha leo ikizingatiwa yuko kwenye fomu nzuri, ambapo alifunga hat-trick wiki iliyopita katika ushindi wa 5-3 dhidi ya Al-Kholood kwenye Ligi Kuu ya Saudi Arabia.
Ronaldo anatarajiwa kurejea uwanjani siku ya Ijumaa, Novemba 6, wakati Al-Nassr itakapovaana na Al Hazem kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Saudi Arabia.





