pmbet

Ronaldo ataka mashabiki wa timu iliyomdhihaki Neves ifungiwe

Sisti Herman

September 13, 2026
Share :

 

Cristiano Ronaldo ametaka kufungiwa maisha kwa mashabiki waliomkejeli mchezaji mwenzake wa timu ya taifa ya Ureno, Rúben Neves, kwa kuimba jina la marehemu Diogo Jota.

 

Tukio hilo lilitokea wakati wa mechi ya Saudi Pro League ambapo timu ya Al-Hilal ilishinda 6-0 dhidi ya Al-Taawoun. Mashabiki wa Al-Taawoun walimlenga kiungo wa Al-Hilal, Neves, kwa kuimba kwa kurudia-rudia jina la "Jota" ili kumuumiza kihisia, wakitumia msiba wa kusikitisha wa aliyekuwa mchezaji wa Liverpool na rafiki yake mkubwa, aliyefariki hivi karibuni kwenye ajali ya gari.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet