Ronaldo atokwa mchozi, Al Nassr ikipoteza fainali ya Kombe la Mfalme
Eric Buyanza
June 1, 2024
Share :
Mshambuliaji nyota wa Al Nassr, Cristiano Ronaldo, jana Ijumaa alilia kwa uchungu wakati timu yake ilipopoteza mchezo kwa penalti 5-4 kutoka kwa Al Hilal kwenye fainali ya Kombe la Mfalme.
Mchezo huo uliisha kwa suluhu ya 1-1 katika muda wa kawaida, na muda wa ziada haukuweza kuipatia timu yoyote matokeo.
Kipa wa Al Hilal, Yassine Bounou aliibuka shujaa wa mchez, baada ya kuokoa mikwaju miwili ya penalti za mwisho za Al Nassr na hivyo kuiwezesha klabu yake kunyakua kombe la mfalme.