Ronaldo atwaa tuzo ya Maradona
Sisti Herman
January 5, 2024
Share :
Mshambuliaji wa Al Nassr FC ya Saudi Arabia, Cristiano Ronaldo ameshinda Tuzo ya Maradona kutoka Globe Soccer kama mfungaji bora wa mwaka 2023 akiwa na magoli 54.
Ronaldo anakuwa mchezaji wa pili kutwaa tuzo hiyo baada ya Mpoland Robert Lewandowski aliyetwaa mnamo 2022.
Ronaldo (38) raia wa Ureno ni mchezaji wa kwanza kutoka Ligi ya Saudi Arabia kutwaa tuzo hiyo.
Ronaldo mwaka 2023;
- Amepokea tuzo ya mfungaji bora Duniani kwa mwaka 2023 kutoka Shirikisho la Kimataifa la Historia ya mpira wa miguu na takwimu Duniani (IFFHS)
- Amepokea tuzo ya Maradona kama mfungaji bora Duniani kwa mwaka 2023 kutoka #GlobeSoccer
- Amepokea tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Desemba 2023 kutoka #SaudiProLeague
Mwezi ujao siku kama ya leo anatimiza miaka 39.