Ronaldo aweka rekodi ya dunia mbele ya Benzema
Sisti Herman
December 27, 2023
Share :
Cristiano Ronaldo jana amefunga magoli mawili ya penati dhidi ya Al Ittihad anayocheza mchezaji mwenzake wa zamani wa Real Madrid Karim Benzema.
Kwa goli 5-2, sasa CR7 amefikisha magoli 53 ndani ya mwaka huu wa 2023, akiwa ndiye mchezaji anayeongoza kuliko wengine wote kwenye utupiaji nyavuni.
Mwaka huu 2023 hawa ndio vinara wa magoli kwenye ligi zote duniani.
1. Cristiano Ronaldo 53
2. Harry Kane 52
3. Kylian Mbappé 52
4. Erling Haaland 50