Ronaldo bado goli 35 tu afikishe goli 1000
Sisti Herman
February 26, 2026
Share :

Cristiano Ronaldo sasa amebakiza hatua ndogo kuingia kwenye historia isiyofutika, akihitaji mabao 35 tu kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya soka kufikisha jumla ya mabao 1,000 katika maisha yake ya soka.
Nyota huyo wa Al-Nassr na timu ya taifa ya Ureno anaendelea kupambana na umri, akikaribia rekodi ambayo wengi waliamini haiwezekani katika soka la kisasa. Kila mchezo sasa umekuwa kama hesabu ya kuelekea kwenye mafanikio hayo ya kihistoria ambayo hayajawahi kutokea.





