Ronaldo haondoki licha ya klabu yake kukosa vikombe
Eric Buyanza
June 1, 2024
Share :
Mkurugenzi Mtendaji wa Al Nassr, Guido Fienga, amethibitisha kuwa Cristiano Ronaldo atasalia katika klabu hiyo msimu ujao licha ya klabu hiyo kumaliza vibaya msimu wa 2023-24.
Al-Nassr imemaliza ikiwa nafasi ya pili kwenye ligi, ikiwa pointi 14 nyuma ya mpinzani wao, Al-Hilal.
Pia walipoteza fainali ya Kombe la Mfalme kwa Al Hilal kwa mikwaju ya penalti siku ya Ijumaa, hii ikimaanisha kikosi hicho kimemaliza msimu bila taji lolote.
Akizungumza na baada ya fainali ya Kombe la Mfalme wa Saudia, Fienga alisema nahodha huyo wa Ureno ataendelea na Al-Nassr na kusisitiza kuwa damu ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39 imekuwa ya njano, akimaanisha rangi kuu ya timu hiyo.