Ronaldo kufanyiwa uchunguzi wa jeraha la misuli
Eric Buyanza
March 2, 2026
Share :
Cristiano Ronaldo atafanyiwa 'vipimo vya dharura' ili kubaini kiwango cha jeraha la misuli alilolipata wakati wa ushindi wa 3-1 wa Al Nassr dhidi ya Al-Fayha siku ya Jumamosi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41 ambaye alikosa penalti wakati wa mchezo huo, alilazimika kuutoka nje zikiwa zimesalia dakika 10 baada ya kulitaarifu benchi kwamba amepata tatizo.
Wengi wanahofia Nahodha huyo wa Ureno anaweza kukosa fainali zake za sita na za mwisho za kombe la Dunia, ikiwa imebaki miezi mitatu tu.






