Ronaldo kusitisha mgomo na kurudi uwanjani Jumamosi
Eric Buyanza
February 10, 2026
Share :

Cristiano Ronaldo anatarajiwa kusitisha mgomo wake kwenye klabu yake ya Al-Nassr na kurejea uwanjani siku ya Jumamosi.
Fowadi huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 41 amekosa mechi mbili kwa sababu hakufurahishwa na jinsi klabu hiyo inavyoendeshwa.
Ronaldo alikuwa kwenye mgomo wa kucheza akidai klabu yake ya Al Nassr haisaidiwi kifedha vya kutosha kama wapinzani wao Al Hilal. Vilabu vyote viwili vinamilikiwa na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia.
Saudi Pro League inaamini ligi yake ni inaendeshwa kwa haki na ufadhili unaotolewa ni wa wazi kwa vilabu vyote.





