pmbet

Ronaldo matatani kwa kumdhihaki mwamuzi

Sisti Herman

November 27, 2026
Share :

 

Nyota wa Al-Nassr, Cristiano Ronaldo, anaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu na Shirikisho la Soka la Asia (AFC), baada ya kufanya ishara iliyozua utata katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Asia dhidi ya Al-Sadd ya Qatar, uliochezwa jana Jumanne, Novemba 24, 2026.

Katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Al-Awwal Park jijini Riyadh, Saudi Arabia, Al-Nassr iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, huku Ronaldo akifunga bao la kwanza kupitia mkwaju wa penalti katika dakika ya 13.

Hata hivyo, mjadala mkubwa baada ya mchezo huo umekuwa kitendo cha Ronaldo kumdhihaki mwamuzi msaidizi kufuatia kutoridhishwa na uamuzi wa waamuzi.

Tukio hilo lilitokea kipindi cha pili wakati Ronaldo alipoamini kuwa alikuwa amefanyiwa faulo ndani ya eneo la hatari na hivyo kuhitaji penalti nyingine. Hata hivyo, mwamuzi msaidizi aliinua kibendera kuashiria kuotea, huku mwamuzi mkuu akitoa faulo kwa upande wa Al-Sadd.

Ronaldo alionekana kukerwa na uamuzi huo, akafunika macho yake kwa mkono na kuiga kitendo cha mwamuzi msaidizi kuinua kibendera, ishara iliyotafsiriwa kuwa ni dhihaka dhidi ya mwamuzi.

Kitendo hicho kinaweza kumuingiza nahodha huyo wa Al-Nassr matatani iwapo AFC itaamua kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yake.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet