pmbet

Ronaldo Mfungaji bora wa ligi kuu Saudi Arabia kwa mara ya pili mfululizo.

Joyce Shedrack

May 27, 2025
Share :

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ureno na klabu ya Al Nassry Criastiano Ronaldo ametwaa kiatu cha mfungaji bora wa ligi kuu ya Saudi Arabia kwa mara ya pili mfululizo.

Cristiano Ronaldo Golden Boot winner 🏆

Nyota huyo ameibuka mfungaji bora wa ligi hiyo baada ya kufunga magoli 25 katika michezo 3 aliyocheza msimu huu huku akitoa pasi 3 za magoli.

 

CR7 mpaka sasa ametwaa tuzo 7 za kiatu cha ufungaji bora wa ligi alizozishinda katika ligi 4 tofauti kuanzia mwaka 2008 alipotwaa akiwa ligi kuu ya Uingereza,Mwaka 2011,2014 na 2015 akiwa ligi kuu ya Hispania Laliga na mwaka 2021 ya ligi kuu ya Italia Serie A huku tuzo mbili akizitwaa msimu jana na msimu huu katika ligi kuu ya Saudi Arabia.

 

Ronaldo amefikisha magoli 800 aliyofunga ngazi ya klabu huku akifunga jumla ya magoli 936 katika maisha yake ya soka.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet