Ronaldo na Mbappe kukutana Robo Fainali Euro 2024
Sisti Herman
July 2, 2024
Share :
Baada ya kuvuka hatua ya mtoano ya 16 bora michuano ya kombe la Mataifa ya Ulaya, Timu za Taifa za Ureno na Ufaransa sasa zitakutana kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo siku ya ijumaa ya julai 5.
Ufaransa imefuzu hatua hiyo baada ya kuwaondoa timu ya Taifa ya Ubelgiji kwa kuwafunga goli 1-0, goli la pekee la Kolo Muani.
Ureno imefuzu hatua hiyo baada ya kuwandoa timu ya Taifa ya Ubelgiji kwa kuwafunga kwa mikwaju ya penalti 3-0 baada ya suluhu ya 0-0 kwenye dakika 120 za mchezo.
Mchezo huo pia utawakutanisha Cristiano Ronaldo na Kylian Mbappe amekuwa akimuangalia Ronaldo kama 'Role Model' wake.