Ronaldo ni mashine, kucheza Saudia sio mwisho - Patrice Evra
Eric Buyanza
August 20, 2025
Share :
Beki wa zamani wa Ufaransa, Patrice Evra, amedokeza iko siku nahodha wa Al-Nassr, Cristiano Ronaldo atarudi kucheza soka la Ulaya.
Itakumbukwa kuelekea mwisho wa msimu wa 2024/2025, kulikuwa na uvumi kwamba Ronaldo anaweza kuondoka Al-Nassr.
Hata hivyo mwezi Juni aliwafunga mdomo wale waliokuwa wakieneza tetesi hizo kwa kusaini mkataba wa miaka miwili na Al-Nassr.
Akizungumza na Stake, Evra alisema: "Cristiano ni mashine. [Saudi Arabia] ni ukurasa mpya tu lakini sio mwisho. Usiseme 'NEVER' kuhusu Ulaya."