Ronaldo yupo sana Al Nassr hadi 2027
Sisti Herman
June 26, 2025
Share :
Nahodha wa Al Nassr, Cristiano Ronaldo amekubali kuongeza mkataba wa miaka miwili na matajiri hao wa Saudi Arabia.
Mkataba wa Ronaldo ulimalizka msimu uliopita na leo amethibitisha kuongeza mkataba hadi mwaka 2027.
Imeelezwa kuwa kulikuwa na mvutano katika makubaliano hayo ambapo Ronaldo alitoa masharti kadha wa kadha ikiwemo ya kuhusishwa moja kwa moja katika usajili wa wachezaji.
Inadaiwa kuwa Ronaldo pia alitaka kocha Stephano Pioli afutwe kazi ndipo aongeze mkataba mpya jambo ambalo Al Nasrr walilikamilisha jana na leo Ronaldo ametangaza kusalia klabuni hapo.