pmbet

Rooney amtolea uvivu Bruno Fernandes, amuita mchoyo asiyejali mashabiki!

Eric Buyanza

October 23, 2026
Share :

Mfungaji bora wa kihistoria wa Manchester United, Wayne Rooney, amewatolea uvivu wachezaji wa klabu hiyo, akiwemo nahodha Bruno Fernandes na Lisandro Martínez, akiwaita "wachoyo" na wanye tabia kama za "watoto wachanga."

 

Mvurugano huo unafuatia kipigo kizito cha mabao 4-1 ambacho Manchester United walikipata ugenini dhidi ya Como kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (Champions League).

 

Baada ya mchezo huo, nahodha Bruno Fernandes alijitokeza hadharani na kuhoji mbinu za kocha Michael Carrick, akidai kuwa benchi la ufundi liliwazuia wachezaji kukaba mmoja kwa mmoja (man-to-man pressing), jambo lililowapa Como mwanya wa kutawala mchezo huo.
 

"Wachezaji hawa wana uchoyo. Hawawajali wachezaji wenzao, hawamjali kocha, wafanyakazi wala mashabiki—wanajijali wenyewe tu," alifoka Rooney.

 

“Mambo yasipoenda wanavyotaka, wanakuwa kama watoto wachanga; wanatupa midoli yao nje ya kigari na kuanza kutupa lawama kwa mtu mwingine yeyote badala ya kujiangalia wao wenyewe.”
 

Rooney aliongeza kuwa hata yeye alikuwa na vipindi ambavyo hakubaliani au hazungumzi na Sir Alex Ferguson, lakini uwanjani alikuwa tayari "kugonga ukuta wa tofali" kwa ajili ya timu. Alimtuhumu Fernandes kwa kutumia lawama hizo kama kichaka cha kuficha kiwango chake kibovu cha sasa uwanjani.

 

Wewe kama shabiki wa Man U, unakubaliana na anachokisema Rooney?

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet