pmbet

Rooney anasema Sir Alex Ferguson ni fundi kuliko Guardiola

Eric Buyanza

June 8, 2024
Share :

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney, amesema bosi wake wa zamani, Sir Alex Ferguson, ana makali zaidi ya Pep Guardiola wa Manchester City linapokuja swala la kupima viwango vyao.

Akiongea katika mahojiano na ESPN Brasil, Rooney alisema;

"Nadhani bila shaka kutakuwa na mabishano kuhusu nani ni bora kati yao, lakini watu huwa wanaangalia tu kile Sir Alex alichokifanya akiwa Manchester United, lakini alichokifanya klabu ya Aberdeen FC kilikuwa cha kustaajabisha," anasema Rooney.

Akaendelea Rooney, “Je Guardiola anaweza kufanya hivyo kwenye timu kama Aberdeen?”

“Bila shaka Guardiola ni bora kwa zama zake na amebadilisha jinsi soka inavyochezwa duniani kote, lakini kwangu bado nasema alichofanikisha Sir Alex, kwenye kandanda ni cha kustaajabisha.”

Ferguson aliifundisha klabu ya Aberdeen Fc ya Scotland kutoka mwaka 1978 mpaka mwaka 1986 na kuipatia mafanikio makubwa klabu hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet