pmbet

Rooney autaka Ukocha United

Sisti Herman

February 29, 2024
Share :

Mshambulaiji wa zamani wa Manchester United na timu ya Taifa ya Uingereza Wyne Rooney kwenye mahojiano maalum na shirika la utangazaji la Uingereza BBC amesema moja kati ya ndoto zake ni kufundisha klabu yake hiyo ya zamani pamoja na Everton.

 

“Bila shaka hilo ndilo lengo langu, Manchester United na Everton ni zote hizi ni kazi ninazojaribu kufika kuzifanya” alisema Rooney alipoulizwa kuhusu lengo la kuifundisha United.

 

Rooney tangu kustaafu kwake mwaka 2021 alianza kujikita kwenye ukocha na hadi sasa amefundisha timu za Deby County, DC United na Birmingham City ambapo kote alikuwa akitimuliwa kwa kupata matokeo mabaya huku akiwa na takwimu hizi, michezo 152, kushinda 41, kupoteza 73 na sare 38.

 

Je kwa uzoefu na takwimu hizo anafaa kufundisha United? weka maoni yako hapo chini

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet