pmbet

Rostam anunua kampuni inayoendesha gesi Songosongo

Sisti Herman

April 14, 2026
Share :

 

Mfanyabiashara, Rostam Azizi kupitia kampuni yake ya Taifa Gas Tanzania Limited, kwa kushirikiana na Amber Energy Investment L.L.C-FZ, wameingia makubaliano ya kununua biashara ya gesi ya kampuni ya Orca Energy Group nchini Tanzania inayomiliki mradi wa Songo Songo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatatu, Aprili 13, 2026, Orca imesaini makubaliano ya mwisho ya ununuzi wa hisa (Share Purchase Agreement) na wanunuzi hao, ambapo itauza hisa zote za kampuni yake tanzu ya PanAfrican Energy Corporation (PAEM), inayomiliki shughuli zake zote za gesi nchini Tanzania.

Chini ya makubaliano hayo, Taifa Gas itanunua asilimia 49 ya hisa za PAEM huku Amber Energy ikichukua asilimia 51, hatua itakayokamilisha uhamisho wa umiliki wa mradi wa gesi wa Songo Songo kwenda kwa wawekezaji hao wapya.

Kulingana na taarifa hiyo Bodi ya Wakurugenzi ya Orca imeeleza uamuzi wa kujiondoa kwenye biashara ya Tanzania umetokana na tathImini ya muda mrefu ya hatari na changamoto zinazokabili shughuli zake nchini.

Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na migogoro inayoendelea, madai mbalimbali, pamoja na kutokuwa na uhakika wa hatIma ya kuongeza muda wa leseni ya maendeleo ya Songo Songo na mikataba ya kugawana uzalishaji (PSA).

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet