Ruben Dias anataka kuchomoka Man City kisa Guardiola kaondoka
Eric Buyanza
May 28, 2026
Share :

Beki wa Manchester City, Ruben Dias, ameripotiwa kumuagiza mwakilishi wake kutafuta uhamisho ili aondoke kutoka Uwanja wa Etihad msimu huu wa joto kufuatia kuondoka kwa kocha Pep Guardiola.
Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 29, alisajiliwa na Man City mwaka 2020 na kucheza jumla ya mechi 255 katika mashindano yote, hajaridhika na mabadiliko ya kiufundi kwa matajiri hao wa jiji la Manchester.
Mkataba wa Ruben unatarajiwa kutamatika mwaka 2029, huku thamani yake ikikaribia euro milioni 60 na tayari Real Madrid, Bayern Munich na Paris Saint-Germain zinamfuatilia kwa ukaribu.





