Rudeboy wa P-Square afunga ndoa
Eric Buyanza
May 25, 2024
Share :
Mwanamuziki Paul Okoye almaarufu kwa jina la 'Rudeboy' anayeunda kundi la P-Square kutoka nchini Nigeria amefunga ndoa ya kimila na mpenzi wake Ifeoma Ivy.
Picha za harusi hiyo zilisambaa kwa wingi mtandaoni siku ya Ijumaa, zikiwaonyesha wanandoa hao wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni ya ndoa.
Haya yanajiri huku kukiwa na uvumi kwamba Ifeoma ana mimba ya mwanamuziki huyo.
Ikumbukwe kuwa mwaka 2004 Paul Okoye alimuoa mwanamke anayeitwa Anita na walijaaliwa watoto watatu kwenye ndoa yao iliyodumu kwa miaka 8.
Mwaka 2021 ndoa hiyo ilivunjika baada ya Anita kudai talaka akimtuhumu Rude Boy kwa usaliti.