Rufaa ya Yanga yatupiliwa mbali
Sisti Herman
December 15, 2023
Share :
Kamati ya usimamizi na uendeshaji wa Ligi Kuu Tanzania bara (TPLB) imetupilia mbali rufaa ya klabu ya Yanga ya kutaka marejeo (review) ya adhabu ya kiungo wake Khalid Aucho ambaye amefungiwa michezo 3 na faini ya Tsh laki tano (500,000) kwa kosa la kumpiga kiwiko kiungo wa Coastal Union Ibrahim Ajibu kwenye mchezo uliochezwa Novemba 08, 2023.
Baada ya kupitia shauri la Yanga na kanuni za Ligi, Kamati ya TPLB imejiridhisha kwa mara nyingine kuwa adhabu iliyotolewa kwa mchezaji huyo ni sahihi hivyo anapaswa kuendelea kuitumikia, huku ikimtaka mchezaji huyo kuzingatia mchezo wa kiungwana wakati wote.