Rulani Amvulia Feitoto Kofia
Sisti Herman
July 30, 2024
Share :
Mara baada ya klabu ya Wydad Casablanca kuitandika 4-1 klabu ya Azam kwenye mchezo wa kirafiki wa maandalizi ya msimu mpya (Pre Season) Kocha wa Wydad AC Rulani Mokwena amekiri kuwa kiungo mshambuliaji wa Azam na timu ya Taifa Tanzania Feisal Salum "Feitoto" ni mmoja wa wachezaji bora na wa kipekee barani Afrika.
"Kwangu katika bara hili (Afrika) Feisal ni mchezaji wa kipekee sana sio tu kama mwanasoka pia napenda utu wake, kiubinadamu ni mtu mzuri sana, pia naipenda Azam FC..." alinukuliwa kocha huyo wa zamani wa Orlando Pirates na Mamelodi Sundwons akiongoa na Azam Tv.
Azam wamehitimisha kambi waliyoiweka Benslimane Morocco kwa mchezo huo wa kirafiki na sasa watarejea Tanzania kwaajili ya maandalizi ya Ngao ya Jamii ambapo watacheza dhidi ya Coastal Union kwenye nusu fainali.