Rulani atambulishwa rasmi kuwa kocha Mkuu Wydad
Sisti Herman
July 11, 2024
Share :
Klabu ya Wydad AC ya Morocco imemtambulisha rasmi aliyekuwa kocha Mkuu wa klabu ya Mamelod Sundowns Rulani Mokwena kuwa kocha wao Mkuu kwa misimu miwili ijayo.
Rulani amejiunga na Wydad wiki moja tu baada ya kuachwa na Mamelod baada ya kuingia kwenye mgogoro na Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo Flemming Berg.