Rulani kuindoka Sundowns, Simba yatajwa
Sisti Herman
July 2, 2024
Share :
Taarifa kutoka vyanzo vya habari mbalimbali nchini Afrika Kusini vimeeleza kuwa kuna nafasi finyu ya klabu ya Mamelodi Sundwons kuendelea kubaki na kocha wao mkuu Rulani Mokwena.
Rulani anadaiwa kuwa kwenye uhusiano usio mzuri na Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo Flemming Berg ambaye inasemekana hamshirikishi Rulani kwenye maamuzi makubwa ya usajili kwa wachezaji wanaoondolewa na kuingizwa.
Wakati hayo yakijiri vyanzo vingine vimemhusisha kunaswa na timu zingine kama Orlando Pirates na Simba ya Tanzania.