pmbet

Rungu la BASATA lamuangukia Madee

Eric Buyanza

December 14, 2023
Share :

Siku moja baada ya msanii Madee kuachia wimbo wake mpya (Nakojoa Pazuri), Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetoa taarifa ya kuufungia wimbo huo kwa kukiuka kanuni za BASATA za mwaka 2018 na mwongozo wa maadili wa kazi za Sanaa wa mwaka 2023.
 

BASATA pia limemtaka Madee aushushe wimbo huo kwenye mitandao ya kijamii na majukwaa ya kidijitali na kuufungia wimbo kutokuimbwa au kuchezwa mahali popote.
 

Madee ametozwa faini ya shilingi Milioni 3 na asifanye shughuli zozote za kimuziki mpaka atakapolipa faini hiyo, huku Producer aliyetengeneza ngoma hiyo 'Mr T Touch' akilambwa faini ya shilingi Milioni 1.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet