Rungu la TFF latua kwa Ally Kamwe.
Joyce Shedrack
April 19, 2025
Share :
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF ) limempa adhabu ya kulipa Sh. Mil Tano Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ali Kamwe.
Kamwe alishtakiwa na Sekretarieti ya TFF akituhumiwa kwa kosa la kuchochea umma kwa ujumla kinyume na Kanuni 73(4) ya Kanuni za Maadili ya TFF Toleo la Mwaka 2021.
Baada ya kusikiliza pande zote na kupitia nyaraka na vielelezo vilivyowasilishwa mbele yake, Kamati imemtia hatiani kwa kosa aliloshtakiwa nalo na kumpa adhabu ya kulipa faini ya kiasi hicho na onyo la kutofanya kosa la kimaadili ndani ya kipindi cha miaka miwili. Adhabu hiyo inaanza tarehe 16/04/2025.
Awali zilitoka taarifa za Kamwe kufungiwa Miaka miwili na TFF kutokana na kosa hilo.